Jeremiah 18:1-6

Katika Nyumba Ya Mfinyanzi

1Hili ndilo neno lililomjia Yeremia kutoka kwa Bwana: 2“Shuka uende mpaka nyumba ya mfinyanzi, nami huko nitakupa ujumbe wangu.” 3Kwa hiyo nikashuka mpaka kwenye nyumba ya mfinyanzi, nikamkuta akifinyanga kwa gurudumu lake. 4Lakini chombo alichokuwa akikifinyanga kutokana na udongo kilivunjika mikononi mwake, hivyo mfinyanzi akakifanya kuwa chombo kingine, umbo jingine kama vile ilivyoonekana vyema kwake yeye.

5Kisha neno la Bwana likanijia kusema: 6 a“Ee nyumba ya Israeli, je, siwezi kuwafanyia kama huyu mfinyanzi afanyavyo?” asema Bwana. “Kama vile udongo ulivyo katika mikono ya mfinyanzi, ndivyo mlivyo katika mkono wangu, ee nyumba ya Israeli.
Copyright information for SwhKC